Msanii Khalifa Ilunga maarufu kama Cp ameamua kuanzisha record label aliyoipa jina la ‘Brain Storm Music’  itakayosimamia kazi zake pamoja na za wasanii wengine.
Katika mahojiano na Times fm msanii huyo amesema amefikia uamuzi huo ikiwa ni katika kuboresha mwenendo mzima wa kazi zake na za wasanii wengine.
“Nafungua label yangu..music label yangu kwa hiyo niko sasa hivi na-register wasanii na vitu kama hivyo.” alifunguka Cp
“Nimeanzisha label yangu ambayo mimi niko chini yake pamoja na wasanii wengi tu ambao wamekuwa wakinifuata, wakiomba ushauri wakiomba miongozo na misaada ya kifedha. Kwa hiyo wote tutakuwa chini ya uongozi mmoja na shughuli zetu za kisanaa zitakuwa zinashughulikiwa na hiyo label.”
Axact

Post A Comment: