posted by Times fm
Bado hali ni tete kwa aliyekuwa daktari wa Michael Jackson, Conrad Murray baada ya rufaa yake iliyokuwa na lengo la kujisafisha akidai kuwa Michael alijiua mwenyewe kukataliwa na mahakama ya Rufaa ya California, hali inayoonesha kuwa kesi hiyo haitapitiwa tena kwa kuwa mahakama hiyo ndiyo mahakama ya juu zaidi.
Dr. Murray ambaye alimaliza kifungo chake baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia, alikata rufaa ili kujisafisha na endapo angeshinda angeweza kurejeshewa tena leseni yake ya kuendesha matibabu kama zamani.
Jaji wa kesi hiyo alisema kuwa madai ya Murray hayakuwa na maana kwa kuwa vipimo vya alama za vidole vilionesha dhahiri kuwa alama za vidole vya Dr. Murray vilikuwa katika kila mahali kwenye chupa ya Propofol, na kwamba hata polisi walipofika baada ya tukio walimkuta Dr. Murray akiwa katika hali ya mtu mwenye hatia.
Ushahidi wa polisi unaonesha kuwa Murray alianza kusafisha eneo la tukio baada ya kifo cha Michael Jackson kabla polisi hawajafika.
Axact

Post A Comment: