Kitendo cha Justine Bieber kutupa mayai katika nyumba ya jirani yake kimezua kizaazaa baada ya kusababisha rafiki yake kukamatwa na madawa ya kulevya (cocaine)siku ya j nne asubuhi akiwa ndani ya nyumba ya Bieber.
Kwa mujibu wa mitandaao ya habari nchini marekani rafiki yake huyo aliyetambulika kwa jina la Lil Za alijikuta anaingia katika mikono ya askari waliofika nyumbani kwa Bieber kwa lengo la kutafuta video yenye uthibitisho wa tukio la kutupa mayai kwa jirani yake.
Habari zaidi zinasema kufuatia hali hiyo maafande waliofika katika nyumba hiyo waliamua kuondoka na kijana huyo na kumuacha Justine Bieber licha ya kuwepo pale ndani na hiyo imeripotiwa ni kutokana na kushindwa kumuhusisha msanii huyo moja kwa moja.
Taarifa zaidi zinasema kesi hiyo inaweza kumpeleka jele Lil Za kwa kipindi cha miaka mitatu.
Post A Comment: