Mtu mmoja anayedaiwa kuwepo katika eneo la tukio na kushuhudia Kanye west akimpiga kijana mwenye umri wa miaka kumi na nane amesema msanii huyu alimpiga kijana huyo kama
mpiganaji wa mchezo wa ngumi anayepigana ili kuua.

Akizungumza na mtandao wa tmz shahidi huyo amesema siku ya tukio kijana huyo baada ya kuzozana na Kim Kardashian alikaa kwenye kiti na ghafla alitookea Kanye west na kuanza kumshambulia kwa makonde katika uso.

Shuhuda huyo ameongeza katika muda wote huo kijana huyo alijitahidi kukinga uso wake ili kuunusuru usidhurike na mashambulizi ya Kanye na kwa muda wote hakuonesha dalili ya kukabiliana na Kanye hali ya kuwa Kanye aliendelea kumshushia kipigo hadi aliporidhika.

Shuhuda huyo aliongeza katika muda wote huo Kanye akiendelea kumtndika kijana huyo mfanya kazi aliyekuwa eneo la mapokezi alikuwa akipiga kelele za kumzuia Kanye lakini msanii huyo hakujali na kuendelea.
Axact

Post A Comment: