Msanii lady Jaydee amewaambia mashabiki wake wanaodhani yeye anatoa mikopo waache imani hiyo kwa ni sikweli na wanaibiwa.
Kupitia ukurasa wake wa face book msanii huyu
anayetamba na ngoma Yahaya amefikia hatua hiyo kufuatia udanganyifu unaofanywa na watu wanaojifanya kuwa ni yeye kwa kutumia jina lake katika mitandao ya jamii na kuwaambia watu kuwa wanakopesha.
Ameeleza yeye hkopeshi na hana mpango huo na kuwatahadharisha watu kuwa makini kwani wataibiwa.
Amefunguka zaidi kwa kusema kama wanahitaji mikopo waende bank ndiko mikopo inakopatikana.
"Watu wanaendelea kuibiwa na wananilalamikia mimi, ndugu zangu wapendwa kuweni makini sana, Mimi sina account yoyote inayotoa mikopo facebook... Kuweni makini, kuweni makini. Narudia tena.
Nawashauri mwende CRDB Bank mkafungue account kama mnataka mikopo/ Bank ndio huwa zinatoa mikopo sio mimi.. Watu ni wezi sana wanatumia majina ya watu kujipatia pesa kwa ulaghai!!!!
Na nyie ndugu zangu mnaoibiwa, hivi tangu lini mikopo ikatolewa facebook???? Nilishaandika zaidi ya mara 3 kuwa sitoi mikopo mi natoa nyimbo na videos tuuu, lakini bado tu naendelea kupewa lawama kuwa nimewaibia watu, Jamaniiii eeeeeh!!
Naskia hiyo page ya Jide wa uongo imetengeneza mpaka tangazo la kwenye TV, humu mjini kuna mambo mengi sana, watu wana njaa zao watafanya kila njia wapate pesa.
Akili kichwani mwako"
Post A Comment: