Ushirikiano katika wimbo mmoja baina ya wasanii wawili wakubwa hapa nchini ambao ni Diamond na Msanii mkongwe professor Jay unazidi kuleta shauku zaidi kwa mashabiki wa muziki hapa nchini baada ya msanii Diamond
kuandika kupitia ukurasa wake wa face juu ya ushirikiano huo.
Msanii huyu ameamua kuwafahamisha mashabiki wake kuwa anafurahia sana collabo hiyo ambayo anafanya na mkongwe huyo.
“Ninapopata Bahati ya kufanya Nyimbo na wakubwa zangu ambao nilikuwa nikiwaskia tangu nawaza Nitoke vipi, hadi leo kupata Fursa kushiriki nao... Hunipa Faraja sana na moyo wa kujituma zaidi....Get ready Kwa hii kitu #KipiSijasikia??? @professourjaytz ft @Diamondplatnumz ... #UsikateTamaa.
Awali msanii Profesor Jay aliandika kupitia ukurasa wake wa face book kuwa kuna ngoma anafanya Diamond kitu ambacho kilivuia watu wengi.
Post A Comment: