Msanii wa muziki hapa nchini Ommy Dimpozi amesema ni ngumu kwa wasanii wa Tanzania kuendeleza muziki wenye asili ya Tanzania kutokana na soko la muziki huo.

Akizungumza bongo20 msanii huyu amesema kuna ugumu sana wa kufanya nyimbo zenye asili ya bongo kutokana na ugumu wa biashara ya muziki huo na ndio maana wasanii wengi wanabadilika kila siku.

Ameeleza ugumu unakuja kuanzia kwa mashabiki wenyewe ambao kwa sasa wengi wao wanataka nyimbo za kuchezeka na zenye mchanganyiko wa ladha mbalimbali za kimataifa.

Sio  rahisi kwa msanii kutoka kwa kuimba mchiriku au mduara na nyinginezo kwani mashabiki wanataka ladha zenye mchanganyiko  wa kimataifa na ndio maana mimi nimechanganya ladha katika wimbo wangu wa tupogo na umefanya vizuri".alisema Ommy Dimpoz

Katika hatua nyingine msanii huyu amesedma atafanya tour katika mikoa ya kanda yaziwa akianzia Kahama mkoani Shinyanga na pia Geita na kisha kurejea kwa ajili ya safari yake nchini Uingereza kwa ajili ya show katika Valentine.

Axact

Post A Comment: