Msanii toka nchini Marekani huenda akajikuta matatani kutokana na kitendo chaa kumshambulia kijana mwenye umri wa miaka kumi na nane.

Kwa mujibu wa mitandao ya habari nchini humo Kanye West amefanya tukio hilo ikiwa ni katika kumsaidia mwenzi wake Kim Kardashian aliyepigia simu mumewe huyo akidai kusumbuliwa na kukashifia na kijana huyo.
Habari zaidi zinasema kuwa kijana huyo alikuwa akimkashifu Kim pamoja na Kanye huku akikumbushia shambulio alilolifanya Kanye dhidi ya muandishi wa habari.
Kufuatia hali hiyo Kim aliamua kumtaarifu mumewe kwa simu na dakika chache baadaye alifika na kuanzisha timbwili.
Kutokana na tukio hilo Kanye ameripotiwa kuingia matatani endapo atapatikana na hatia.
Axact

Post A Comment: