Muandaaji wa muziki hapa nchini anayefanya shughuli zake jijini Mwanza Deey Classic amewashauri maproducer wengine kuwa wabunifu ili kutengeneza
beat ambazo hazina ufanano na zilizowahi kutumika.
Akizungumza na bongo20 msanii huyu amesema hivi sasa kumekuwa na udanganyifu katika utengenezaji ambapo producers wana sample beat hali ambayo inashusha muziki wetu.
Akielezea sababu za utengenezi huo producer huyu amesema kunatokana na watu wasio na ujuzi na uwezo wa uandaaji wa muziki kutaka kutengeneza beathali ambayo inawafanya wajikute wanaendelea ku sample na sio kubuni zao.
Amesema ni vyema kwa waandaaji kutambua wanachokifanya na kuwa wabunifu ili kuandaa kazi za kipekee.
Post A Comment: