Msanii Wa Muziki Hapa Nchini Soprano Amewashauri Wasanii
Wanaotaka Kutoka Kutumia Fursa Inayopatikana Katika Mitandao Mbalimbali Ili
Kutangaza Muziki Wao.
Ameeleza watu wanatumia facebook,twitter,whats up kujitangaza
na kutangaza muziki wao hivyo hakuna haja ya kuendelea kufikiria namna ya
kujitangaza.
“sasa hivi kuna mitandao ya kijamii na kuna blogs
tofautitofauti hivyo ni vyema wasanii wanaotaka kujitangaza wakawasiliana na
watu wa blogs ili kusambaza kazi zao kwa urahisi.”
Katika hatua nyingine msanii huyu Ikiwa ni katika kuvunja
ukimya wa tangu mwaka 2010 ameachia wimbo mpya unaoitwa “Turn your lights down
low na kueleza kuwa wimbo huo ni kama zawadi
kwa mashabiki wa muziki.
Post A Comment: