Msanii mkongwe na mmoja wa waasisi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Joseph Haule ama Profesa Jay yupo mbioni kutoa wimbo mpya akiwa na Diamond.

 Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa face book msanii huyu ameposti picha inayomuonesha yeye mwenyewe,Producer mkongwe P funk majani na na Msanii Diamond.
Post yake hiyo inasomeka kama ifuatavyo hapo chini

"Ndani ya Bongo Records with the Super dupa producer P - funk Majani and @diamondplatnumz himself Muda Huu # COOKING for all yall'.... kaeni mkao wa kula watu wangu!!!

Taarifa hii ya msanii huyu imeonekana kupokelewa kwa kwa furaha na kuleta shauku kwa baadhi ya mashabiki ya kutaka kuusikia wimbo huo 

Hatua hii ya Profesa Jay inakuja ikiwa ni baada ya kuwa kimya kidogo kwa upande wake na akionekana kung'ara katika nyimbo za kushirikishwa.
Axact

Post A Comment: