Msanii wa muziki hapa nchi Tunda man amesema kuna haja ya kuwepo na ushirikiano baina ya watangazaji na wasanii katika kupinga vitendo vya wizi wa kazi za wasanii.
Akiongea kupitia kipindi cha Extra Vaganza cha Afya radio amesema kutokana na unyonyaji wa kazi za wasanii ni muda sasa umefika kwa watu wote wanaohusika kutoa taarifa kwa jamii( watangazaji) kupigia kelele swala hili ili kulitokomeza.
Pia msanii huyu hakuishia hapo kwani amewageukia wapenzi na mashabiki wa muziki kwa kuwaomba kukataa kununua kazi zisizo original ili kuwaunga mkono wasanii wa Tanzania. Ameeleza vitendo vya ku burn cd feki kuna endelea kutokana mashabiki wenyewe kuendelea kununua cd za aina hiyo.
Ameongeza kuendelea kwa vitendo hivi kunawafanya wasanii kutofaidika na jasho lao na badala yake wana faidika watu wengine.
"Kwa mfano katika nchi za wenzetu mashabiki wanaona furaha kununua Cd origina ili kuwa sapoti wasanii wo na ndiyo maana wanaendelea. Alisema tunda man.
Katika hatua nyingine msanii huyu amewaomba mashabiki wake kuendelea kuisapoti ngoma yake mpya aliyofanya na Ali kiba.
Post A Comment: