Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Nasib Abdul au Diamond amesema anatarajia kuwasomesha watoto watatu ambao wameshinda katika
shindano la kucheza wimbo wake wa My number one. Kupitia ukurasa wake wa Face book msanii huyu amepost picha inayomuonesha akiwa na mmojaa kati ya watoto walioshinda sambamba na kuandika yeye na kampuni yake watawasomesha watawasomesha watoto hao ikiwa ni pamoja na kuwahamisha kutoka shule wanazosoma sasa kuwapeleka katika shule zenye ubora wa juu zaidi.
"Mmoja ya watoto watatu walioshinda kucheza ngololo.management yangu ya WCB itawasomesha miaka yote waliyobakiza shuleni ikiwa ni pamoja na kuwahamishia katika shule zilizo bora zaidi....Ahsanten sana Daresalaam kwa sapoti mliyonipa jana ...."
Post A Comment: