NEY WA MITEGO: SIKUWA NA MAWAZO NA TUZO ZA KTMA
Msanii Ney Wa Mitego amesema hakuwa
amezichukulia kwa umuhimu tuzo za Kilimanjaro music award licha ya kupata tuzo.
Akizungumza na muandishi wetu
msanii huyu amesema tuzo hizo hazikuwa kwenye akili yake na kuwa aliamua
kuendelea na shughuli zake za kimuziki mkoani Mbeya kwa mujibu wa ratiba yake.
Ameongeza kwa kuwa wamegundua
kuwa ana uwezo mkubwa kimuziki na hata kumpa tuzo ni jambo zuri na la
kumshukuru Mungu.
Vilevile msanii huyu akatoa
shukurani kwa mashabiki kwa kumpigia kura na kuwaomba waendelee kuwa naye kwani
bila wao yeye sio kitu.
Mbali na hilo msanii huyu amesema
yeye na Diamond wapo katika harakati za tour ya muziki gani ambayo wanatarajia
kuzunguka karibu mikoa yote Tanzania.
Post A Comment: