JOSLIN : NAFURAHISHWA SANA NA USHINDANI ULIOPO KWENYE GEMU YA MUZIKI BONGO FLEVA
Msanii wa muziki wa
kizazi kipya Joslin amesema anafurahishwa na ushindani aliopo kwanye muziki wa
bongo fleva kwani unamfanya msanii kufikiria zaidi ni namna gani anaweza
kuboresha zaidi kazi yake.
Joslin amesema
ushindani huu unaleta changamoto kwa wasanii ukilinganisha na kipindi kile
ambacho wasanii walikuwa wachache na hakukuwa na ushindani mkubwa.
Ameeleza hivi sasa gemu
imebadilika inalipa tofauti na zamani na inahiaji akili ya ziada na endapo mtu hatokuwa makini lazima atapotea.
Kuhusu ukimya wake
Joslin amesema umetokana na kutingwa na shughuli nyingine pia kujipanga kwani
sanaa inahitaji utulivu na huwezi kutoa ngoma kila siku.
Mbali na hilo pia
msanii huyu amewaomba mashabiki wake kukaa tayari kumpokea tena kwani yuko
mbioni kuachia ngoma mpya.
Post A Comment: