TIMBULO : "SINA MAKOSA" SIKUUTUNGA KWA AJILI YA JACK
Msanii wa bongo fleva Timbulo
amesema wimbo wa SINA MAKOSA anaotamba nao hivi sasa hakuutunga kwa ajili ya kumuimbia
aliyekuwa mpenzi wake Jack Pentezel.
Timbulo amesema licha
ya wimbo huu kuwa na story ya ukweli ndani yake lakini haikuwa kwa ajili ya
Jack isipokuwa kuna mpenzi wake mwingine ambaye alidai hata akimtaja hatuwezi
kumuelewa kwani si maarufu.
Amesema kwa sasa hana
mpango wa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na watu maarufu kwani anajua
matatizo yao.
Amesema kwa bahati
nzuri nyimbo zake nyingi zina uhalisia na ameimba kwa hisia kwa hivyo hakuna
sababu kwa mashabiki wake kufikiria hivyo.
Timbulo amesema haya
baada ya swali aliloulizwa na muandishi wa blogu hii lililotokana na kuwepo kwa
tetesi kuwa aliutunga kwa ajili ya kumbembeleza mpenzi wake huyo wa zamani.
Msanii huyu amesema
hivi karibuni anatarajia kuachia video ya wimbo huo.
Post A Comment: