PRODUCER
WA “DEAR GOD” DEEY CLASSIC AMESEMA
MENSEN ALISTAHILI TUZO
Producer wa muziki wa
kizazi kipya hapa nchini anyefanyia shughuli zake jijini Mwanza Deey Classic
amesema Producer Mensen Selector wa defertality music aliyekuwa mshindani wake alistahili kuchukua tuzo
katika kipengele cha producer anayechipukia.
Akizungumza katika
kipindi cha hot mix cha EATV hapo jana producer huyu amesema kutokana na kufahamika
kwa Mensen sambamba na uwingi wa kazi alizofanya kufahamika na kupata air time kumefanya
apate tuzo hiyo kwa urahisi.
Amesema
kilichomuangusha yeye ni kutofahamika sana kwa watu kutokana na kutotokea sana
katika medias licha ya kusikika kwa jina lake katika baadhi ya nyimbo ambazo
amezifanya.
Mbali na hilo mproducer
huyu amesema yeye anajiamini na kuwa haoni tabu kufanya kazi katika mkoa wowote
tofauti na Dar es salam kama ilivyo kwa maproducer wengi.
Akizungumzia producer
anayemkubali alisema anatamani kuwa kama producer P funk wa bongo recrd kutokana na ubora
wa kazi zake.
Deey Classic
ametengeneza nyimbo nyingi kama Dera God iliyochukua tuzo tatu pia beat ya
wimbo wa msanii young killer aliowashirikisha Stamina na Quick Racka “Jana na
leo” na nyingine nyingi.
Post A Comment: