RATIBA
YA MAZISHI YA MSANII LANGA
KILEO
Mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa hiphop Tanzania Langa Kileo
unatarajiwa kuzikwa mapema juma tatu ya wiki ijayo majira ya saa kumi jioni
mara baada ya shughuli za kumuaga zitakazoanza siku hiyo majira ya saa saba
mchana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia blogu hii ni kuwa msiba wa marehemu upo nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hosp ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production.
Itakumbukwa sana nyota ya marehemu Langa ilianza kuonekana na kung'ara kupitia shindano la cocacola pop star ambapo kwa Tanzania alikuwa ni mmoja kati ya washindi watatu ambao waliunda kundi la pamoja lililojulikana kama WAKILISHA.
Katika kundi hilo alikuwa yeye, Witness pamoja na Shaa ambao walifanikiwa kutoa heat kama hoi na Swanglish na baadae kila mmoja kufanya kazi zake kama solo artist.
Post A Comment: