BAADA YA KUDAIWA KUKASHIFU MSIBA WA MAREHEMU NGWEA MSANII OMMY DIMPOZ AFUNGUKA YA MOYONI
Msanii Ommy Dimpozi amesema sababu ya kuandikwa
vibaya katika vyombo vya habari imetokana na kushindana kibiashara.
Akizungumza kupitia kipindi Cha Extra Vaganza cha
Afya radio Mwanza leo hii msanii huyu amesema hali hiyo imesababishwa na yeye kukataa
kufanya show iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya vyombo vya habari (jina tunalihifadhi ) ambapo amedai malipo
yalikuwa chini ukilinganisha na matakwa yake.
Kufuatia hali hiyo Ommy Dimpoz ameeleza kampuni hiyo
iliamua kumuandika vibaya kwa lengo la kumchafua kama moja ya sehemu ya
kumkomoa ili wakati mwingine asipingane nao.
Ameeleza amesikitishwa sana na hali hiyo kwani
kilichoandikwa si kweli na kuwa kimetengenezwa ili kumdhoofisha.
Ameongeza yeye kama msanii sanaa ni kazi yake na
kuwa anafanya kwa ajili ya maslahi kama ilivyo kwa watu wengine wanapokuwa
katika ofisi zao na kuwaomba mashabiki wamuelewe na kutomchukulia vibaya.
Mapema wiki hii kumekuwepo na taarifa zinazodai kuwa
Ommy Dimpoz amekuwa na dharau na pia kiburi hata kukashifu wenzie kutokana na kuwa
mmoja kati ya wasanii walio kwenye chati ya juu kwa sasa.
Juhudi za kuwatafuta wahusika kuzungumzia swala hili
zinaendelea.
Post A Comment: