SAJNA: NEY WA MITEGO ANAUFAHAMU
WIMBO
WA "MPIRA GANI"
Msanii wa Bongofleva Sajna
aliyewahi kutamba na nyimbo kama Iveta sitaki kuumizwa na nyingine nyingi amesema
wimbo wa MPIRA GANI aliyotumia style na melody ya wimbo wa Muziki gani,mmiliki
wake anaufahamu.
Akizungumza mwishoni
mwa wiki hii msanii huyu alisema kabla ya kuufanya wimbo huo alimtaarifu Ney ambaye ndiye mmiliki na kuruhusiwa kuufanya
kwa ajili ya mashabiki.
Amesema watu wamekuwa
wakidhani kuwa alikurupuka bila kutoa taarifa na hivyo amewaomba waelewe hivyo
na endapo kukitokea hawataamini ni ruksa kumtafuta Ney na kumuuliza.
Akizungumzia kwanini
ameamua kutumia style na melody ya wimbo huo amesema ilitokana na mapendekezo
yaliyotolewa na watu wake wa karibu ambao walimshauri afanye hivyo kama zawadi
kwa mashabiki na haikuwa kwa ajili ya kuuachia kama ilivyo sasa.
Sajna amesema hivi karibuni anatarajia kuachia rasmi ngoma mpya ambayo ilipangwa kutoka kabla ya MPIRA GANI
“kuna wimbo ambao
natarajia kuuachia hivi karibuni nimewashirikisha Ben Pol na C- sir Madin kwa
hiyo mashabiki wakae yatari kunipokea” alisema Sajna.
Post A Comment: