AFANDE SELE :
MUZIKIUNAKUA,WASANII WANASHUKA
Msanii wa bongo fleva aliyewahi
kuwa mfalme wa Rhymes hapa bongo Suleiman Msindi au Afande sele amesema wakati muziki
wa bongo ukipanda wasanii wa muziki huo wanashuka.
Msanii huyu amesema
kiwango cha muziki nchini kinazidi kukuwa kwa maana ya kupata nafasi zaidi
katika jamii ukilinganisha na mwanzo wakati muziki huo ukionekana wa kihuni.
Ameongeza hivi sasa
wasanii wanapata nafasi ya kufanya kazi na wasanii wa nje na kupata mafaniko ukilinganisha
na mwanzo ambapo wasanii walilipwa pesa kidogo na hawakuwa wakifahamika sana
nje.
Ameeleza tatizo
lililopo katika muziki huu kwa sasa ni kuwa wasanii wanashuka kiuandishi kwa
maana ya kuandika mashairi mepesi ukilinganisha na nyuma ambapo walitumia
akilizaidi katika uandishi wa nyimbo zao.
Msanii huyu amewahi
kutamba na nyimbo kama Darubini,Watu na pesa Acha kupiga mayowe na nyingine
nyingi na ni mmoja kati ya wasanii wakongwe wanaoheshimika kwa utunzi na uandishi wa mashairi.
Post A Comment: