WASANII DOGO JANJA NA DOGO D WAFUNGUKA MAGUMU WALIYOKUTANA NAYO
Msanii dogo D kutoka kundi la Wakubwa wa jiji amewashauri wasanii ambao hawajatoka kujiamin na kutokata tamaa kutokana na vikwazo wanavyokutana navyo.
Kupitia show ya Extra Vaganza ya Afya radio msanii huyu amesema wasanii wengi wamekuwa wakishindwa kuhimili vishindo vya majaribu na kupoteza ndoto zao kitendo kinachowafanya waendelee kuhangaika mtaani hali ya kuwa wana vipaji.
Akitolea mfano wa aliyokutana nayo Dogo D amesema aliwahi kubaniwa kurekodi kwa kisingizio cha umri na mengine mengi ikiwamo kudharauliwa, hata hivyo hakukata tamaa na kuendelea mbele kitendo kilichoanza kumpa mafanikio leo.
Kwa upande wake Msanii Dogo janja amewaomba mashabiki wa muziki kuthamini wasanii wa nyumbani na kuwasapoti ili kuwatengenezea maisha.
Amesema kwa upande wake yeye nyumbani Arusha anapata sapoti kubwa hivyo angependa kuona na wengine wakipewa sapoti katika mikoa yao kama anayoipata yeye.

Post A Comment: