MSANII RACHEL AWAFUNGUKIA WASANII WADOGO  


 



Msanii Rachel toka nyumba ya vipaji THT amewashauri wasanii wanaoingia kwenye game ya muziki kutowashirikisha wasanii wakubwa na badala yake watoke wao kama wao.

 Akizungmza na muandishi wa blogu hii hivi karibuni msanii huyu amesema kitendo hicho kinawafanya waonekane wamepewa lifti (wanabebwa) na wasanii hao.

Ameeleza ni vyema wakajipanga na kutoka wao kama wao ili kuuonesha uma kuwa wana vipaji na wanaweza bila kubebwa.

" mfano kama mimi namshukuru Mungu kwani nimeweza kutoka na kukubalika bila kumshirikisha msanii mwingine hivyo hata wao wanaweza".

Ameeleza wasanii wengi humfuata wakiomba wamshirikishe kwenye nyimbo zao lakini huwa shauri waimbe wao kama wao ili kujitengenezea taswira nzuri kwa mashabiki.

Pia akamshauri msanii Shilole kuwa safari hii asishirikishe msanii mwingine na atoke yeye kama yeye ili aoneshe ubora wake kwani alipofikia hivi sasa anaweza kufanya yeye kama yeye .

Axact

Post A Comment: