Jeshi la polisi
katika kanda maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawasaka watuhumiwa watano wanaotajwa kuhusika kubaka
wasichana wawili katika eneo hilo.
Kamanda wa polisi
wa kanda hiyo, Andrew Satta amesema
tukio la kwanza mwanafunzi wa shule ya msingi Kibasisi iliyopo kwenye kijiji cha Kangariani wilayani Tarime
(jina limehifadhiwa), alibakwa na watu wawili wakati akirejea nyumbani kutoka
shuleni siku hiyo ya machi 26.
Kamanda Satta ameeleza
kuwa, mwanafunzi huyo alikutana njiani na watu wawili waliokuwa wamejifunga
vitambaa vyeusi usoni, ambao walimkamata kwa nguvu, kumburuza vichakani na
kumbaka kwa zamu wakiwa wamemfunga kitambaa mdomoni.
Baada ya kumaliza tukio
hilo walitokomea kwenye vichaka na kutorokea mahali pasipojulikana .
Katika tukio la
pili, usiku wa siku hiyo katika kijiji cha Ruhu
kwenye mwalo wa wavuvi wilayani rorya, msichana mwenye umri wa miaka 21 (jina
limehifadhiwa), alidanganywa na vijana wanne kuwa aliitwa na rafiki yake wa
kiume, jambo lililomfanya awaombe wamsindikize alipo na walitii.
Kamanda Satta amesema bila kujua nia ya vijana
hao kumdanganya hivyo, binti huyo ambaye hata hivyo anawatambua na kufahamu
majina yao, alikubali na kuondoka nao.
Alisema kuwa baada
ya kufika kwenye eneo la mwalo wa wavuvi, karibu na vichaka, huku kukiwa na
giza nene, waliamua kumbaka kwa zamu na kumwacha akiwa hoi vichakani,
Post A Comment: