Wakazi wa vijiji vya ukanda wa Igombe na Kayenze wilayani Ilemela
mkoani Mwanza wamesema kufunguliwa kwa baabara inayounganisha maeneo hayo na Mwanza
mjini kupitia uwanja wandege kumesaidia sana kutatua changamoto ikiwemo swala
la huduma za afya.
Kabla ya kufunguliwa kwa barabara
hiyo wakazi hao walisema walihangaika kufikia huduma za afya kwa kuwa
walilazimika kutembea umbali mrefu pia kupanda kwa nauli hli iliyowaweka katika
wakati mgumu.
Mbali na hivyo wamesema walikabiliwa
na adhabu mbalimbali ikiwemo vipigo kutokana na kutumia barabara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongela
amesema bada ya kukamilika kwa zoezi la kufungua barabara hiyo hivi sasa
wanashughulikia swala la nauli.
Naye meneja wa wakala
wa barabara (Tanroad) mkoa wa Mwanza injia Leonard Kadashi amesema tayari wamekwishaanza
mpango wa kuikarabati barabara hiyo.
Kushughulikiwa kwa barabara hiyo
kunaondoa malalamiko na adha za muda mrefu walizopata wakazi hao.
Post A Comment: