Diwani wa kata ya Mtema
wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Veronica
Kanyanhila amejikuta akiwekwa rumande kwa tuhuma za kupingana na serikali
juu ya kipindupindu ambapo yeye anaunga mkono kuwa ugonjwa huo unatokana na
imani za kishirikina.
Habari zaidi
zinasema zaidi ya wakazi mia sita themanini wa kijiji cha Lusungo kilichopo
katika kata hiyo wamekuwa wakijisadia vichakani hali inayopunguza kasi ya
kukabiliana na ugonjwa huo.
Mkuu wa wilaya ya
kyela Thea Ntara ameamuru
kushikiliwa kwa diwani huyo akidai ameshindwa kusimamia usafi sambamba na
kumtolea kauli mbaya pindi alipomuuliza juu ya swala hilo.
Kisa hicho
kimetokea wakati mkuu huyo wa wilaya alipoembelea makazi yenye utata katika
kata hiyo.
Naye fisa afya wa
wilaya hiyo Godfrey Balosi amesema diwani huyo amekuwa akisimamia imani kuwa
ugonjwa huo ni uchawi huku akishindwa kuhamasisha watu kujenga vyoo na kuweka
mazingira katika hali ya usafi.
Post A Comment: