Augustin Ollomi kamanda wa polisi mkoa wa Kagera
Mwanaume mmoja mkoani kagera amejikuta matatani baada ya kumshambulia mkewe kwa ngumi na mateke hadi kusababisha kifo chake.
Habari zaidi zinasema mwanaume huyo alfonce abyalimana aliamua kutokomea kusikojulikana kuukwepa mkono wa sheria baada ya kubaini kuwa amesababisha kifo cha mkewe.
Kamanda wa polisi mkoani kagera Augustine Ollomi alisema ukio hilo lilitokea march 27 mwaka huu katika kijiji cha nyamihaga wiayani ngara na kumtaja mwanamke aliyeuawa kuwa ni janeth abyalimana (36).
Kamanda ollomi alisema polisi bado inaendelea na jitihada kumsaka bwana huyo ili kumfikisha katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Katika hatua nyingine mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la georgina emmanuely (68) alikutwa ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mwili wake kutelekezwa shambani mwa felician andrew.
Tukio hilo lilitokea machi 27 katika kata ya ijumbi wilayani muleba mkoani kagera ambapo chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.
Tayari polisi mkoani humo wanamshikilia mwanaume mmoja johansen sebastian (39) kwa mahojiano zaidi kuhusu tukio hilo.
Mwili wa marehemu umechukuliwa na ndugu zake na kufanya maziko baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Axact

Post A Comment: