Baadhi ya wakazi wa
mtaa wa Nyasaka B jijini Mwanza wapo hatarini kuathirika kiafya
kutokana na kutumia maji ya mto kutpikia na kunywa.
Wakazi hao wanasema
maji yalitoka siku chache mara baada ya kuripoti taarifa yao juu ya uhaba wa
maji katika eneo hilo na baadaye kutoweka.
Baadhi ya wakazi katika
eneo hilo wanasema kwa sasa wako njiapanda
hali inayowalazimu kunywa maji ya mtoni.
Kwa kuwa tatizo hilo
lipo kwa muda mrefu na bado hakujapatikana suluhu ya kudumu, wenyeji wa eneo
hili wanatamani kuhama kwa kuwa wanahisi kuwa wameachilizwa na serikali.
Jembe fm inaendelea na
jitihada kuwasiliana na uongozi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira
kujua hatua zilizopo kwa sasa.
Post A Comment: