Wakala wa
Golikipa wa Manchester United, Victor Valdes amesema hajafanya
mazungumzo yoyote na klabu ya Uturuki ya Antalyaspor, lakini
amethibitisha kuwa timu hiyo inawinda saini ya Mhispania huyo.
Wakala
huyo anayeitwa, Gines Carvajal amesema: “Nimekuwa na mawasiliano na watu
mbalimbali kutoka Uturuki wakitaka mazungumzo ya kumsajili Victor, lakini
sijaongea na rais wa klabu ya Uturuki”.
Akuzungumza
zaidi na AS ameongeza: “Sijui. Sina mpango wa kuzungumza na mtu yeyote
kwasababu mchezaji hajavutiwa kwenda Antalyaspor.
“Anatamani
kuendelea kubakia Manchester United na amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba
wake”.
“Hatuoni
sababu ya kuondoka klabuni hapo. United ni miongoni mwa timu mbili au tatu bora
zaidi duniani.
‘Victor
anajipanga kupigania nafasi ya kuanza msimu ujao na anahitaji kuisaidia timu
kadri atavyoweza”.
Post A Comment: