Mlinzi wa kilabu ya Manchester City Martin Demichelis ameshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza kwa madai ya kucheza kamari.
Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 anatuhumiwa kwa kukiuka sheria 12 zinazohusiana na mechi kati ya tarehe 22 na 28 Januari 2016.
Demichelis ana hadi Aprili 5 kujibu shtaka hilo dhidi yake.
Hatahivyo hakuna pendekezo la iwapo shtaka hilo linahusiana na mechi 25 za ligi na kombe la ligi ambazo ameshiriki msimu huu.
Sheria mpya zilizoanza kutekelezwa msimu wa 2014-2015 zinamaanisha kuwa wachezaji na makocha wanazuiliwa kushiriki kucheza dau katika mechi yoyote duniani.
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lina uwezo ya kumpiga faini ama hata kumpiga marufuku mtu yeyote atakayekiuka sheria.
Axact

Post A Comment: