MAJANGA ILINIPA DILI SOUTH AFRIKA



Msanii wa muziki na filamu hapa nchini Snura Mushi maarufu kama Snura amesema wimbo wa majanga ulimpa dili la kufanya filamu nchini Afrika kusini.

Akifunguka hivi karibuni msanii huyu amesema dili hilo lilikuja mara baada ya waandaaji wa filamu mpya inaayoitwa Tandeka nchini humo kumuona akishoot video ya wimbo wake huo wa Majanga na kuvutiwa naye.

Ameeleza baada ya hapo walimtafuta na kumuita kwenye usahili na baada ya kufaulu walimpa nafasi ya muhusika mkuu.

Imeelezwa kuwa filamu hiyo imetumia lugha mbalimbali zikiwemo Kiswahili, Kizulu na Kiingereza.
Axact

Post A Comment: