Walimu
wa kuu wa shule za msingi mkoani geita wametakiwa kutoa taarifa za walimu
wanaoacha kufundisha na kuendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda
wakati wa masomo.
Habari
kutoka mkoani humo zinasema walimu wa shule za msingi wamekuwa wakiacha
kufundisha watoto na badala yake kwenda kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo
kuendesha pikipiki hizo.
Afisa
elimu mkoa wa geita efrancia bachuma amsema hali hiyo haikubaliki na kuwa
walimu wakuu watoe taarifa ili walimu hao wachukulie hatua za kinidhamu.
Ameongeza
vitedo hivyo vinawaathiri wananfunzi kwa kuwa hawapati masomo kama
inavyostahili.
Kwa
upande wao baadhi ya wanafunzi wamesema hali hiyo imewafanya kushindwa kufaulu
katika masomo yao.
Post A Comment: