Baadhi ya wajumbe
wa umoja wa vijana wilaya ya nyamagana mkoani mwanza wamemtaka mwenyekiti wa
umja huo hussein kimu kuuomba radhi umoja huo kutokana na taarifa yake kwa
vyombo vya habari ikisema umoja huo unamtuhumu kiongozi edward lowasa kuandaa
vijana kwa ajili ya kufanya fujo mjin dodoma.
Mmja wa wajumbe
hao omari juma yahya ambaye ni
mwenyekiti wa vijana kata ya mirongo amesema wao hawahusiki na kauli hiyo na
kuwa anapaswa kuomba radhi.
Ameongeza kinyume
na hivyo huenda wajumbe hao wakafanya maamuzi magumu.
Naye mjumbe
mwingine kutoka katika umoja huo amesema mbali na kuomba radhi anapaswa kufuta
kauli aliyoitoa kwa vyombo vya habari sambamba na kushughlikia maswala
yanayohusu umja huo.
Mapema wiki
iliyopita mwenyekiti wa umoja huo hussein kimu alimshutumu aliyekuwa mtia nia wa
kuwania mbio za uraisi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ccm edward lowasa kuwa alifanya mpango wa kuandaa vijana wakiwemo mabaunsa ili kufanya vurugu Dodoma endapo jina lake litakatwa.
Bongo 20 na Jembe habari
vinaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Hussein kimu mwenyekiti wa umoja wa
vijana wa ccm ili kuzungumzia shutuma hizo.
Post A Comment: