Baadhi ya wananchi
wa mtaa wa S.D.A uliopo kata ya isamilo jijini mwanza wamesema wako njia panda
kutokana na kutojua sababu za kujiuzuru kwa mwenyekiti wa mtaa huo.
Wananchi hao
wamesema hali hiyo imewaathiri kutokana na kumtegemea kwa kiasi kikubwa katika
shughuli za mtaa wao.
Wameongeza ni
vyema angeweka wazi jambo lililomfanya kuachia madaraka hayo .
Kwa upande wake
kaimu mwenyekiti wa mtaa huo amesema sababu kubwa iliyomfanya kuachia madaraka
ni kutokana na kuhama makazi na kupata ajira katika eneo jingine.
Kukosekana kwa
wenyeviti wa mitaa katika baadhi ya maeneo kumeelzwa kurudisha nyuma maendleo
ya mitaa hiyo.
Post A Comment: