BEN POL AONGEA BAADA YA KUINGIA KWENYE TUZO MPYA ZA YOUTH FOR AFRICA UNDER 30 YEARS KWA 2013
Baadaya kuingizwa
kwenye tuzo za youth for Africa katika kipengele cha burudani msanii Ben pol
amesema hali hiyo inamfanya kuongeza bidii zaidi katika kazi zake.
Akizungumza na
muandishi wetu leo hii msanii huyu amesema tuzo hizo zimemtia moyo zaidi na
kuahidi kufanya vizuri zaidi kwa ajili ya mashabiki wake.
Licha ya kuwa bado
hajajua kama tuzo hizo zitahitaji kura za mashabiki amewaomba mashabiki kukaa
tayari kwa lolote kwa ajili ya kumsapoti na endapo ikitokea mshinidi atahitaji
kura za watu basi wampigie.
Wasanii wengine
walioingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Vanesa Mdee Lina na
Michael Mlingwa.
Hivi karibuni msanii
huyu amekuwa ni mmoja kati ya wasanii walioibuka na tuzo katika tuzo za
Kilimanjaro music Award.
Post A Comment: