DRAKE AONESHA NIA YA KUMALIZA BIFU NA CHRISS BROWN
Msanii Drake mzaliwa wa
Canada anayeshika na wimbo wa start from the bottom ameamua kurudi nyuma na
kutaka kukaa chini na Chriss brown kumaliza tofauti zao.
Kwa mujibu wa mtandao
wa Mtv Drake aliliambia jarida la GQ kuwa ana mpango huo ili warudi katika hali
waliyokuwa nayo awali.
Habari zaidi zinasema
Drake alisema kuwa hawezi kumzingua mtu hadi pale atakapo zinguliwa.
Aliongeza zaidi kuwa
anahitaji kuelekeza nguvu zake kwenye albamu yake ijayo na sio bifu lisilo na
manufaa kati yao.
Ugomvi wa mastaa hawa
ulitokana na Chriss kumshutumu Drake kutembea na mpenzi wake wa zamani Rihana
na itakumbukwa watu hawa wamewahi kufanyiana fujo katika club ya usiku huko new
York Marekani.
Post A Comment: