Baada ya kuwepo kwa shauku ya mashabiki wa muziki katika nchi mbali mbali dunian ya kutaka kujua jina la mtoto wa Kanye west na kim kardashian  kunataarifa zimetoka zinazoweka wazi jina la kichanga hicho.
Kwa mujibu wa mtandao wa tmz wa nchini Marekani jina la mtoto huyo limepatikana kupitia Chanzo cha kuaminika kilichokaribu na familia hiyo.

Mtandao huo umesema mtoto huyo anaitwa North Est  na hii ni baada ya kupata maelezo toka kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo  huko Cedars-Sinai hospital in Loss Angeles Marekani.

Taarifa zaidi zinasema jina hili limetokana na familia ya Kanye kwa upande wa mama yake aliyekuwa akiitwa Donda West.

Habari hizi zinakuja baada ya usiri uliotawala baina ya wazazi hawa Kanye na Kim juu ya kutoa taarifa za kichanga chao


Axact

Post A Comment: