ZOEZI LA UOKOAJI WA NDEGE 

LILILOTIKISA JIJINI MWANZA



Ambulance ya waokoaji wakiwa Airport Mwanza  na baadhi ya askari


Leo baadhi ya wanachi jijini Mwanza wamejikuta katika wasiwasi mkubwa baada ya kupata taarifa kuwa kuna ndege imeanguka ziwani jijini humo na ilikuwa ikitokea Bujumbura na ilikuwa na abiria 50.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika toka uongozi wa juu zinasema hakuna ajali yoyote iliyotokea isipokuwa kulikuwa na zoezi la uokoaji wa ajali za ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwanza likiwa na lengo la kupima utayari wa idara za uokoaji kama vile hospitali, jeshi la zimamoto, jeshi la polisi na wananchi kwa ujumla.

mkurugenzi wa kiwanja cha ndege cha mwanza  Ester Madare amesema katika zoezi hilo walikuwa wakiangalia vyombo hivyo vitafika wakati gani na madhara kiasi gani yanaweza kutokea.

Amesema ndege iliyoandaliwa ilikuwa na abiria hamsini walioandaliwa na wote wakiwa na ujuzi wa kuogelea huku mmoja kati yao aliigiza amefariki na zoezi lilianza saa nne na dakika 17 asubuhi na na kumalizika saa sita mchana.

Nao baadhi ya mashuhuda wa zoezi hilo ambao pia wameshiriki katika uokoaji wamesema zoezi hilo limeenda vizuri na idara zote za uokoaji zimejitahidi kuwahi kutoa huduma.

Mashuhuda wengine wametoa kasoro baadhi ya idara zilizo na boti ziendazo kasi kwa kutofika kwa wakati lakini pia umeonekana upungufu wa  boti hizo.

Mpaka waandishi wa Afya radio Mwanza IDDI JUMA NA NOEL THOMPSON  wanaondoka uwanjani hapo tathimini ya utendaji wa zoezi kwa  idara husika ilikuwa bado haijafanyika na meneja wa uwanja huo amesema tathimini hiyo itatolewa pindi itakapokamilika.
Axact

Post A Comment: