Muandishi wa Afya radio Harith Jaha akizungumza na mkazi wa Kisesa katika kisima wanachorumia kuteka maji




Muandishi wa Afya radio Iddi Juma akifanya mahojiano na mkazi wa kisesa



Baadhi ya wakazi wa mji wa Kisesa wilaya ya magu mkoani Mwanza wapo hatarini kupatwa na magonjwa yanayotokana na utumiaji wa maji yasiyo salama.Wakizungumza na kipindi cha Kurunzi cha Afya radio Mwanza walisema wanalazimika kutumia maji hayo kutokana uhaba wa maji unaowakabili. Waliongeza kuwa mji huo umekuwa akikabiliwa na uhaba wa maji ambapo tegemeo lao kubwa ni visima ambavyo kuna wakati navyo hukauka na kufanya tatizo kuwa kubwa zaidi. "Mabomba yapo lakini ni machache na pia yanatoa maji kidogo na kwa muda mfupi yani unaweza kuja saa kumi na mbili asubui ukatoka saa saba mchana na wakati mwingine adi saa kumi kutokana na foleni ya ndoo" Alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.Kufuatia kero hiyo kipindi hicho kilimtafuta afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini mwanza Bw.Robert Masunya ambaye alikiri kujua tatizo hilo na kuwaomba wakazi hao kuwa wavumilivu kwa kuwa tayari mpango wa kupeleka maji eneo hilo umekwishaa na tayari wamekwisha tandaza bomba hadi katika eneo la Kanyama kuelekea Kisesa.Kwa ujumla wakazi wa mtaa wa Kisesa wana hali ngumu katika huduma ya maji kutokana na upungufu wa mabomba pia uchakavu wa miundombinu ya mabomba na hata visima visivyokuwa salama.




Axact

Post A Comment: