Jaji wa Los Angeles ametoa uamuzi wa kuendelea kwa kesi ya Kanye West na Kim K dhidi ya mmoja kati ya waanzilishi wa YouTube, Chad Hurley aliyevujisha video ya tukio la wawili hao kuvishana pete.
Mara ya kwanza Jaji wa mahakama ya California alisitisha kwa muda kuendelea kwa kesi hiyo baada ya Chad Hurley kudai kesi hiyo dhidi yake ifutwe kwa kuwa katiba inamlinda kwa madai kuweka kipande cha video hiyo ilikuwa sehemu ya ‘haki/uhuru wa kujieleza’.
Hurley alifunguliwa mashtaka siku moja baada ya kuweka kwenye mtandao wake wa MixBit kipande cha video ya tukio hilo lililofanyika October mwaka jana, kinyume na makubaliano au masharti yaliyowekwa na Kanye West na Kim Kardashian kuwa picha wala video hazirusiwi kuchukuliwa wakati wa tukio.
Katika mashtaka hayo, Kanye West na Kim Kardashian wamedai kuwa Hurley alivunja makubaliano ya usiri yaliyowekwa na kwamba inawezekana amevunja haki ya waandaaji wa show ya ‘Keeping Up With The Kardshians’ ambao walikuwa wanakibali cha kushuti tukio hilo na kulionesha kwenye kituo cha runinga cha E!
Kim Kardashian na Kanye West wanataka walipwe fidia ambayo bado hawajataja kiwango. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 17, Mwaka huu.
Axact

Post A Comment: