Huenda hali hii ikawa fundisho kwa baadhi ya viongozi hapa nchini ambao wamekuwa wakitajwa kuwa miongoni mwa watumiaji wa vilevi na pia kuonekana katika club za usiku.Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC Meya wa mji wa Toronto Rob Ford ambaye amekuwa akijikuta katika mazingira magumu kufuatia utumiaji wake wa vilevi na mihadharati ameripotiwa kujitambua na kupanga kuchukua likizo ili kufanyia kazi tatizo hilo.Taarifa kutoka kwa mwanasheria wa meya huyo Bw.Denis Moris zinasema tayari meya huyo amekwisha tambua tatizo linalomdhalilisha na kuwa atachukua likizo ili kulifanyia kazi.Uamuzi huu wa meya huyo unakuja katika wakati ambao magazeti mawili ya Canada yakidai yamepata kanda mpya ya inayomuonesha meya huyo akiwa amelewa na akitoa maneno mabaya kww wanawake na wanasiasa wenzake. Habari zaidi zinasema meya huyo bado anampango wa kutetea nafasi yake katika uchaguzi October mwaka huu.






Axact

Post A Comment: