Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amesema atatumia nguvu kuwaondoa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wanaopanga bidhaa zao katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika mapema jijini Mwanza mapema wiki hii Ndikilo alisema walikwisha fanya mazungumzo na wafanya biashara hao ili waondoke lakini zoezi hilo halijafanikiwa.
Kufuatia hali hiyo alieleza hakuna namna zaidi ya kuwaondoa kwa nguvu akitumia jeshi la polisi. Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi mkoani Mwanza Christopher Fuime alisema kabla ya kuanza kuwaondoa watatoa matangazo ya kuwataka waondoke na kisha kuwatoa kwa nguvu wala watakao kaidi.
Post A Comment: