Wafanya usafi wa barabara na madampo jijini mwanza
wapo katika hatari ya kuathirika kiafya kutokana na baadhi yao kufanya shughuli
hiyo bila ya kuwa na vifaa vinavyotakiwa.
Akizungumza na Afya radio bi Amina Almas mmoja wa wafanya
usafi jijini humo alisema wengi wao wanakabiliwa na upungufu wa vifaa kama
gloves,viatu vya usalama na vifaa vya kuzuia vumbi ambapo alieleza kuwa baadhi
yao wanavyo na wengine bado hawajapatiwa.
Alieleza kuwa hulazimika kuzoa taka kwa mikono na vifaa
visivyo rasmi kama ubao ambapo hukutana na changamoto ya kukutana na vinyesi na
hata wanyama waliogongwa na vyombo vya usafiri.
Kwa upande wake Afisa
afya wa jiji la Mwanza Bw. Danford Kamenya alisema wao kama wasimamizi wa
masuala ya afya wanafanya jitihada za kuwabana mawakala wa usafi ambao ndio
waajii wa wafanya usafi hao ili kufuata taratibu zinazotakiwa
Vilevile Bw. Kamenya aliwaomba wafanya usafi huo walio na vifaa kuvitumia na sio kuviacha nyumbani
Post A Comment: