Producer Charles Francis aka C9, ambaye ndiye mmiliki wa studio za C9 ameeleza kuwa baada ya kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kumiliki studio yake mwaka jana, hivi sasa ana ndoto ya kukua na kuanzisha shule ya muziki.
Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, producer C9 ameeleza kuwa pamoja na kufundisha mambo mengine ya muziki, shule hiyo itafundisha pia utayarishaji wa muziki. Hii ni ndoto ya C9.
“Kwa hiyo baadae nimepanga kama itawezekana na ntakuwa na uwezo basi tufungue shule nzuri tu ya masuala ya muziki itakayowafundisha kuanzia wasanii na maproducer pia.” Amesema C9.
Mtayarishaji huyo ameeleza kuwa studio yake inawasaidia sana wasanii chipukizi kupata kazi nzuri kwa kuwaelekeza hadi hatua ya mwisho wakiwapa muda mwingi wa kufanya kazi katika studio hiyo (studio time).
C9 alikuwa mkali wa The Jump Off kwa wiki hii, na alielezea safari yake ya muziki hadi alipofikia hatua ya kumiliki studio yake mwenyewe.
Post A Comment: