Rehema Chalamila yuko tayari kurudi kwa nguvu kwenye kiwanda cha muziki huku akipingana na baadhi ya fikra za wadau wengi wa muziki kuwa albam hailipi kuliko kutoa wimbo mmoja mmoja kwa sasa, yeye amepanga kuitoa kwa ajili ya watu wake waliommis.

Lakini kabla albam haijatoka, mkali hiyo aliyewahi kuahidi mara kadhaa kuwa atarudi jukwaani na amewamiss watu wake, ataachia single kadhaa baada ya albam yake anayoiandaa hivi sasa kukamilika.

Akionesha kurudi katika hali yake kiafya na kifikra pia, Ray C amepanga kuja na kitu kingine ambacho ni ‘foundation’ yake na bila shaka itakuwa inahusu muziki na kuwatoa wasanii wachanga.

Mkali huyo ameweka wazi mpango wake kupitia Instagram kwa kupost picha iliyoandikwa ‘Ray C Foundation’, na kuipa maelezo ‘Coming Soon’
Axact

Post A Comment: