boMeneja mkongwe ambaye pia ni msimamizi wa kundi kubwa la muziki la ‘Wanaume Family’ kutoka Temeke, Said Fella ameeleza kuwa yeye katika muziki wa Tanzania sio mwanamuziki bali kuna muda anaamua tu kuingia studio na kufanya yake kwa lengo la kuuzingua tu muziki.

Fella ambaye ana mradi mpya wa Mkubwa na Wanawe, amesikika kupitia kipindi cha ‘Trending Africa’ cha 100.5 Times Fm alipoulizwa kuhusu uhusika wake kwenye game kama mwanamuziki kwa kuwa ameshawahi kuachia track hewani.

“Mimi ujue sio kwamba naamua kufanya muziki, ila kuna muda tu nakaa nasema bwana ngoja nipeleke ladha kwa mashabiki wetu, ndo maana natoaga ile ladha tu. Mimi sio kwamba mimi ni mwanamuziiiki, hapana. Mimi nasimamia muziki bana, lakini sio mwanamuziki, ila kuna muda huwa nauzinguazingua tu muziki.” Amesema Said Fella.

Ameeongeza kuwa yeye huwa anafanya ngoma muda mwingine kwa lengo la kufurahisha watu tu na kuwaonesha wanamuziki wake kuwa anapokuwa anawaelekeza vitu kwenye muziki wajue anajua kweli na sio kwamba hafahamu.

“Sifanyi kubahatisha kufanya muziki, yaani niliamua kuingia kufanya muziki kama nilikuwa mimi ndiye meneja wa kwanza Tanzania niliangalia muziki unafanya hivi, kwanza nilianza kuusoma mimi mwenyewe mpaka nikaanza kuusimamia. Ndio maana hadi leo ni mwaka wa 14 niko kwenye usimamizi wa muziki.”

Mwaka 2012, Fella alianza kufanya muziki wa aina ya Taarabu na kutangaza kuwa ataachia albam nzima ya nyimbo za aina hiyo.
Axact

Post A Comment: