Msanii toka nchini Markani Roby Rihana Fenty amesema kuwa alikuwa akipenda kvaa mavazi ya kiume ili awe na muonekano wa nusu jinsia ya kike na nusu jinsia ya kiume.
Akifunguka katika interview na jarida maarufu la Vogue la nchini Marekani msanii huyu amesema wakati yupo mdogo alipendelea sana hali hiyo hasa alipokuwa na umri wa 13 na 14.
“Nilipokuwa na umri wa miaka 13 au 14, sikuwa nataka kuvaa nguo ambazo mama yangu alikuwa anataka nivae. Nilikuwa napenda sana muonekano wa kivulana. Marafiki zangu wote walikuwa wavulana. Nilikuwa napenda vitu ambavyo wavulana wanafanya.” Alisema Rihanna.
Mbali na hilo msanii huyu amedai kuwa hakupenda kuwa maarufu licha ya kupenda kuimba tangu akiwa mdogo ambapo ameeleza alijibidiisha na mazoeziya kuimba mara kwa mara ili kuboresha sauti yake.
“Nilikuwa naimba sana kama mtoto, sana. Nilifanya mazoezi sana kuitengeneza sauti yangu. Napenda kuimba. Nilipenda na haikuwa ratiba ya kila siku. Sikupenda kuwa maarufu. Nilitaka tu muziki wangu usikike duniani kote. Kisha ikatokea na ikaja na umaarufu.” Rihanna aliliambia jarida la Vogue.
Post A Comment: