Baada ya kuibuka kwa story inayomzungumzia msanii Lady
Jaydee kuanza mafunzo ya Karate ameamua kufunguka kwa ksema kuwa ni kwa ajili
ya kujiweka fiti.
Akizungumza na times fm msanii huyo amesema hakuamua kuingia
katika mafunzo hayo ili kukabiliana na mtu.
“Hapana ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio
kwa ajili ya kutaka kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo
likitokea ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza.
Wiki iliyopita habari ya msanii huyu kujiunga na mazoezi
hayo ilitawala katika vyombo mbalimbali vya habari kiasi cha kuzua mijadala kwa
baadhi ya mashabiki wa muziki juu ya sababu za msanii huyu kujiunga katika
mafunzo hayo.
Post A Comment: