Msanii Tunda man kutoka nchini Tanzania amesema amejikuta ana
mvuruga msanii msanii kutoka nchini Uganda Jose Chameleon baada ya kumpa beat
yenye mahadhi ya Vanga.
Msanii huyu ameeleza kuwa alimpa beat hiyo ikiwa ni katika
mpango wake wa kufanya wimbo na msanii huyo ambapo Chameleon baada ya kuisikia
beat hiyo alishikwa na mshangao na asijue ataimbaje.
Katika hatua nyingine msanii huyu amesema ili kuboresha kazi
za wasanii hapa nchini kunahitajika kitengo kitakachosimamia kazi hizo kwa kuzikagua
ubora wake.
Akifunguka kupitia kipindi cha Hot mix cha Eatv msanii huyu
amesema kinachochangia kuporomoka kwa ubora wa kazi ni kukosekana kwa kwa
kitengo hicho hali ambayo inamfanya kila msanii kufanya anachoona ni sawa hata kama anapotea.
“
Unajua pale kwetu tuna kitengo kinachopitia kazi zetu
ndomaana zinakuwa na ubora tofauti na wengine ambao wanatengeneza kazi kasha
wanawapa washkaji zao wazisikilize ambapo hata kama
ina makosa wao wanaisifia” alifungka msanii huyu
Ameongeza baraza la sanaa Tanzania (Basata) hallikagui ubora
wa kazi zaidi ya kusajili wimbo.
Post A Comment: