Siku
chache baada ya diamond kushutumiwa kumuandika vibaya msanii mwenzake ali kiba
ameamua kuvunja ukimya na kuelezea hisia zake.
Kupitia
ukurasa wake wa face book msanii huyo ameandika maelezo yanayoashiria kusikitishwa
na shutuma hizo huku akiwataka wasanii kuacha kumzushia na badala yake
kufikiria namna ya kuliletea taifa heshima kwa kutengeneza muziki mzuri.
Tazama
alichokiandika hapo chini
“kiukweli,
nasikitishwa sana jins baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea
ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti nimewatusi
kwenye media, mara sjui nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu....kwanini wanamuziki
wa tanzania tunashindwa kubadilika... Mbona mi nahangaika na muziki wangu
kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui
"sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya
"sina tatizo"... Sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua
kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu
na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka
kazi! Aliandika diamond.
Hivi
karibuni msanii huyu amekuwa akihusishwa kuwa katika bifu na msanii ali kiba
ambapo hadi hivi sasa kila mmoja ametajwa kumuandika mwenzie katika mitandao ya
kijamii.
Post A Comment: